CHINI ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves, msafara wa Yanga SC umerejea Dar Februari Mosi kutoka Zanzibar baada ya kukamilisha dakika 90 zakimataifa.
Januari 31,2026 Yanga SC 1-1 Al Ahly ulikuwa mchezo wa hatua ya makundi CAF Champions League ikiwa ni mchezo wa nne kwa wababe wote wawili.
Yanga SC kwenye kundi D ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 5 kibindoni msimu wa 2025/26 na vinara ni Al Ahly.
Mchezo ujao Yanga SC itakuwa ugenini dhidi ya AS Far yenye pointi 5 pia ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo.Mshindi wa mchezo ujao atakuwa amefungua ukurasa wa kutinga hatua ya robo fainali.
Kwenye mchezo uliopita nyumbani Uwanja wa New Amaan Complex goli la Yanga SC lilifungwa na beki Ibrahim Bacca dakika ya 45.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.