Simba SC 2-2 de Tunis hali ni tete kimataifa, robo fainali yamoto

KATIKA kundi D Simba SC inaburuza mkia ikiwa imekusanya pointi moja baada ya mechi 4 2025/26. Matokeo haya yanadidimiza malego ya Simba SC kutinga hatua ya makundi kutokana na kukusanya pointi kiduchu baada ya mechi nne ikisaliwa na mechi mbili.

Mahesabu yanawagomea Simba SC kutinga hatua ya robo fainali ikiwa Esperance watapata matokeo kwenye mchezo ujao hivyo matumaini ni hafifu kwa msimu huu wa 2025/26.

Februari Mosi 2026 ubao umesoma wa Uwanja wa Mkapa Simba SC 2-2 Esperance ni matokeo ya mchezo wa nne Uwanja wa Mkapa.

Shomari Kapombe dakika ya 39, Yusuph Kagoma dakika ya 45 walifunga kwa Simba SC huku Waarabu wakipindua meza dakika ya 64 kupitia kwa Aboubacar Diakite na Kouceilia dakika ya 79, Februari Mosi 2026.

Kagoma kiungo wa Simba SC ni mchezaji bora wa mchezo kutokana na kiwango ambacho amekionyesha huku nyota wa Esperance H. Jelassi akikosa pigo la penalti.
Umiliki wa mpira ni 57/43
Jumla mashuti ni 8/11
Kipa kuokoa 3/1
Kona ni 4/1
Faulo 14/14
Kadi za njano 3/0

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.