BREAKING: MASHABIKI WA SIMBA WAPATA AJALI KAHAMA, SITA WAJERUHIWA

Gari iliyokuwa imebeba mashabiki wa klabu ya Simba SC wa ‘tawi la Wekundu wa Chalinze’ kutoka Kahama kwenda mkoani Kagera imepata ajali katika kijiji cha mwendakulima kwenye hifadhi ya serikali ya msitu wa mkweni. Mashabiki hao walikua wanaenda kushudia mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa hapo kesho katika uwanja wa Kaitaba.