Singida Black Stars Yafanya Mabadiliko Makuu: Ouma Kocha Mkuu, Najjar Meneja Mkuu

Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kumteua kocha David Ouma kuwa kocha mkuu mpya klabuni hapo akichukua nafasi ya Miguel Angel Gamondi ambaye imembadilishia majukumu na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu.

Taarifa ya leo Januari 05, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa Ouma ambaye awali alikuwa kocha msaidizi atashirikiana na Makocha Wasaidizi Mousa Nd’aw na Muhibu Kanu.

Vilevile Singida Black Stars imemwajiri Othmen Najjar kuwa Meneja Mkuu wa Timu hiyo huku ikimbadilishia majukumu Ramadhani Nsanzurwimo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi na kumteua kuwa Mshauri wa Ufundi wa klabu.

Aidha klabu hiyo imebainisha kwamba haina pingamizi lolote kwa Kocha Miguel Gamondi kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa kudumu wa Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars), endapo mamlaka husika zitaona inafaa.