TFF YAFUNGUKIA ISHU YA BOSI SIMBA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeweka wazi kwamba halijamfungulia kesi, Polisi kiongozi yoyote wa mpira wa miguu.

Ilikuwa inaelezwa kuwa Ofisa Mtendaji wa Simba, Barbara Gonzalez amefunguliwa mashataka Polisi na kiongozi mmoja wa TFF.

Mashtaka hayo ilielezwa kuwa yamefunguliwa katika kituo Kikuu Cha Polisi, Dar, Januari 20,2022 ambapo Barbara alipokea wito wa kufika kituoni hapo na baada ya kufika aliwekwa ndani kwa saa nane kisha kusomewa shtaka lake.

Shtaka linalomkabili Barbara ni kutoa lugha isiyopendeza kwa kiongozi mmoja ambaye aliwazuia siku ya Desemba 11 2021 katika mchezo kati ya Yanga na Simba.

Kwenye mchezo huo Simba ilitoshana nguvu bila kufungana na Yanga na waliweza kugawana pointi mojamoja.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa masuala yote yanayowahusu viongozi wa mpira wa miguu yamekuwa yakipelekwa kwenye vyombo vinayohusika na mpira.