BAADA ya jana Januari 23 Yanga kuweza kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Polisi Tanzania,Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amefungukia kuhusu sakata la beki wao Djuma Shaban kuonekana akimpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania.
Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Djuma dakika ya 89 alionekana akimchezea faulo mchezaji wa Polisi Tanzania na mwamuzi wa kati hakuweza kuona tukio hilo ambalo lilikuwa ni baya.
Manara amesema kuwa kitendo ambacho amekifanya sio kizuri na wenyewe wanakikemea.
“Yes sio kitendo kizuri na Yanga tunakikemea hata kama kulikuwa na provocations,(hasira)”.
Baada ya kitendo hicho, Djuma alifanyiwa mabadiliko kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13 za ligi na haijapoteza mchezo hata mmoja.