AZAM FC WAINYOOSHA PRISONS 4G, AJIBU AKIWASHA

TANZANIA Prisons wana kazi ya kujipanga upya baada ya kukubali kunyooshwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Mabao ya Azam yalifungwa na Tepsie Evance dakika ya 27’, Ismail Kada dakika ya 69’, Ibrahim Ajibu  dakika ya 71’ na Charlse Zulu 83.

Ajibu aliingia kwenye mchezo huo akitokea benchi na aliweza kusababisha kupatikana kwa bao la pili baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa kisha likakutana na Kada.

Kada ambaye aliwahi kucheza ndani ya Prisons baada ya kufunga bao hilo aliomba msamaha lakini hakuweza kufuta bao hilo lililoongeza hali ya kujiamini kwa Azam FC.

Ajibu aliweza kufunga bao lake la kwanza baada ya kujiunga na Azam FC ikiwa ni muda mfupi baada ya kuvunja mkataba wake ndani ya Simba.