Iran 2-0 Tanzania, mchezo wa kirafiki wa kimataifa

HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa makosa binafsi yameigharimu timu kupoteza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Iran.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Iran 2-0 Tanzania, mabao yakifungwa na Amirhossen Hosseinzadeh dakika ya 17 kwa mkwaju wa penalti na Mohammad Mohebi dakika ya 26.

Morocco amesema kuwa walianza kwa kutengeneza nafasi kupitia kwa kiungo Feisal Salum lakini alikosa kufunga mwisho wapinzani wakapata nafasi wakatumia.

“Tulikuwa na mchezo mgumu na mapema tulipata nafasi tukashindwa kutumia. Makosa ya mtu mmojammoja yalitokea na hapo wapinzani wetu wakapata nafasi wakatumia.

“Kipindi cha pili tulikuwa imara lakini tulishindwa kutumka nafasi ambazo tulitengeneza. Wapinzani walitupa presha kubwa ilikuwa hivyo lakini ni matokeo ya mpira, “.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao upo katika kalenda ya FIFA uliochezwa Uwanja wa Rashid, Dubai, Oktoba 14 2025.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.