Simba SC imetinga fainali Muungano Cup

Simba SC imetinga hatua ya fainali Muungano Cup 2026 kwa ushindi wa magoli 3-0 Mlandege FC. Kituo kinachofuata fainali ni Yanga SC vs Simba SC, Aprili 29, 2026.

Magoli ya Simba SC katika nusu fainali ya pili Aprili 26,2026 yamefungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 61, Anicet Oura dakika ya 76 na Maema dakika ya 89.

Simba SC itakutana na Yanga SC kwenye fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.

Yanga SC ilianza kutinga hatua ya fainali kwa ushindi wa magoli 2-1 Azam FC mchezo wa Dar Dabi uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Neo Maema ametwaa tuzo ya mchezaji bora akipewa zawadi ya milioni moja kutoka Zanzibar School of Health na Hussein Mbegu ametwaa tuzo ya mchezaji aliyeonesha mchezo wa kiungwana akizawadiwa laki 5 kutoka City Institute of Health Dar es Salaam.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.