LIGI KUU BARA KUENDELEA MBEYA,PALEPALE SOKOINE

 LEO Januari 18 kutakuwa na mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara ambapo Mbeya Kwanza itawakaribisha Azam FC kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine.

Itakuwa ni saa 10:00 jioni, ambapo uwanja huo jana ulitumika kwa Mbeya City kuweza kuitungua Simba bao 1-0 ambalo lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 19.

Mbeya Kwanza iliyo nafasi ya 11 na pointi zake kibindoni ni 11 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya 7 na pointi zake ni 15.

Huduma ya nyota wake Crispin Ngushi ambaye amesajiliwa na Yanga huku Azam FC ikiwa na ingizo jipya moja ambalo ni Ibrahim Ajibu lililokuwa linakipiga ndani ya Simba.