>

KIUNGO MPYA WA YANGA HESABU ZAKE KUBWA KWELI

CHICO Ushindi kiungo mpya ndani ya kikosi cha Yanga ameweka wazi kwamba hesabu kubwa baada ya kuwa ni mali ya Yanga ni kuweza kuipa ushindi timu hiyo kwenye mechi ambazo watacheza.

Ushindi ni moja ya usajili mpya kwenye dirisha dogo na alitambulishwa Tanga, Uwanja wa Mkwakwani wakati ubao uliposoma Coastal Union 0-2 Yanga.

Kiungo huyo amesema:”Hakuna furaha kubwa kwangu zaidi ya kuona kwamba timu inashinda na hilo lipo wazi hasa kutokana na timu iliyopo.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi nimewaona namna ambavyo wanapenda timu yao na kushangilia muda wote hili ni jema na kila mmoja anapenda kuona inakuwa hivyo.

“Ambacho ninaweza kuahidi ni ushirikiano na wachezaji wenzagu pamoja na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi katika kufanya mambo mazuri kwa ajili ya timu,”.

Winga huyo anachukua nafasi ya Mukoko Tonombe ambaye yeye anakwenda TP Mazembe kwa makubaliano maalumu kwa mujibu wa taarifa.

Licha ya kwamba Mukoko kuelezwa kwamba bado anahitaji kuitumikia Yanga hakuna namna muda wake wa miezi sita anaweza kuimalizia akiwa TP Mazembe.