LEO Januari 17 imepangwa droo ya Azam Sports Federation Cup, (ASFC) ikiwa ni hatua ya 32 bora kwenye mashindano haya.
Simba ambao ni mabingwa watetezi waakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Dar City kwenye mchezo unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Yanga wao watacheza na Mbao FC mchezo huo nao utachezwa pia Uwanja wa Mkapa na matarajio ya mechi hizo kuchezwa ni kati Januri 27-31 na hatua ya 16 bora inatarajiwa kuchezwa kati ya Februari 12-17.
Pia Biashara United v Mbeya Kwanza, African Lyon V Kagera Sugar,African Sports v Mtibwa Sugar, KMC v Ruvu Shooting, Baga Friends v Catamine FC.
Tanzania Prisons v Rhino Rangers,Mbuni FC v Lipuli,Pamba FC v Stand United,Azam FC v Transit Camp, Coastal Union v Top Boys, Namungo FC v Lindi United.
Dodoma Jiji v Sumbawanga United, Polisi Tanzania v Ndanda FC na Geita Gold v Tunduru Korosho ambapo washindi wa hatua.
hii ya 32 bora hao wataibukia kwenye 16 bora Ni Abeid Mziba,’Telelo’ na Maalim Saleh hawa wamechangaya balls kwenye pots na kuweza kuonesha karatasi zenye majina ya timu na ilikuwa lve Azam TV.