KMC KAMILI KUIVAA TANZANIA PRISONS

TANZANIA One,kipa bora wa muda wote Juma Kaseja kuhusu mchezo wa kesho Januari 16 dhidi ya Tanzania Prisons ameweka wazi kwamba wanahitaji pointi tatu.

Kaseja ni nahodha wa KMC kesho anatarajia kuwaongoza wachezaji wenzake katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya 13 na pointi 11 baada ya kucheza mechi 11 na Prisons ipo nafasi ya 12 na pointi 11 tofauti yao ni mabao ya kufunga na kufungana.

Prisons imefunga mabao 8 na KMC imefunga mabao 9 kwa upande ya yale ya kufungwa Prisons imefungwa 12 na KMC 14.

Kaseja amesema:”Tunajua kwamba wao wapo nyumbani na wanahitaji pointi tatu hata sisi tunazihitaji, likini sisi tumazihitaji zaidi hasa ukizingatia nafasi ambayo  tupo.

“Mashabiki wamekuwa pamoja nasi ninaomba wazidi kuendelea kuwa pamoja nasi kwani wachezaji tupo tayari na tunajua kwamba ushindani utakuwa mkubwa,”.