FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema kuwa kwa msimu wa 2024/25 wamejitahidi kupambana na kufikia malengo licha ya kushindwa kutwaa ubingwa watafanya maboresho kwa msimu ujao.
Kuna asilimia chache kwa Fadlu kubaki ndani ya kikosi cha Simba SC msimu wa 2025/26. Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba SC unafanya mazungumzo na kocha huyo ili aendelee kubaki ndani ya kikosi hicho.
Rekodi zinaonyesha kuwa baada ya kuongoza mechi 30 ni ushindi kwenye mechi 25, sare 3 na imepoteza mechi 2. Mechi hizo mbili ni Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC.
Kwenye mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC na mzunguko wa pili, Yanga SC 2-0 Simba SC. Ni mabao matatu Simba SC imefungwa huku Yanga SC ikiwa haijafungwa.
“Tulikuwa na msimu wenye ushindani mkubwa na kwa kiasi chake tumefikiwa malengo licha ya kutokufurahia yale ambayo yametokea. Kushindana na Yanga SC tukiwa na wachezaji ambao bado nwanazidi kuimarika inatupa nguvu kujipanga zaidi kwa wakati ujao.
“Tutazungumza na uongozi kuona namna yakufanya maboresho katika kikosi. Ninawapongeza mashabiki kutokana na kuwa nasi kwenye kila hatua.”
Mabingwa wa ligi ni Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Pointi zao kibindoni ni 82 huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 83. Simba SC nafasi ya pili pointi 78 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 69.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.