ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa msimu wa 2024/25 wamepitia mengi il ani siri yao ya mafanikio. Yanga SC ni mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25 ikiwa ni taji lao la 31 na wamepanga kulipeleka Ikulu..
Mchezo namba 184, Yanga SC ilishinda mbele ya Simba SC. Juni 25 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC.
Kamwe amebainisha kuwa kutakuwa na supu ya ngamia, Juni 26 na dua maalumu kwa ajili ya kutwaa ubingwa makao makuu ya timu Jangwani.
“Msimu huu tumepitia mengi sana kama Klabu. Lakini siri yetu ya mafanikio. Licha ya mawimbi makubwa ni umoja na mshikamano umetusaidia. Viongozi ambao tuliwaamini watusaidie kwenye nyakati ngumu wamefanikisha hilo na tumevuka salama.
“Bila kusahau mchango wa viongozi wote wa matawi, mashabiki na wanachama tunasema asante sana.
“Kijana yoyote anayemaliza kidato cha nne mwaka huu basi atakuwa amepata fursa ya kushuhudia Klabu ya Yanga ikishinda mataji manne mfululizo, tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia ushindi huu mkubwa.
“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake thabiti kwa taifa letu. Usalama na amani umesaidia sisi kucheza mpira katika mazingira rafiki. Ubingwa huu ni zawadi kwa Rais. Tunalenga kupeleka ubingwa huu Ikulu kuonesha kuwa tumeridhishwa sana na uongozi wake.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.