ZIKIWA zimebaki siku mbili kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, KMC FC kupitia ofisa habari wake, Christina
Mwagala wameweka wazi mchakato wao wa usajili.
Dirisha dogo la usajili lilifunguliwa Desemba 16, 2021 kwa kushirikisha timu za Ligi Kuu Bara, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake na kutarajiwa kufungwa Januari 15, 2022.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mwagala amefunguka kuwa:
“Bado hatujafanya chochote kuhusiana na usajili, sisi kawaida yetu huwa tunasajili kimyakimya, kwa maana hiyo ikitokea tumefanya
usajili au mabadiliko yoyote itajulikana.”