MABEKI WA YANGA WAELEKEA TUNISSIA

ABDALAH Shaibu beki wa kati wa Yanga ameelekea Tunissia kwa ajili ya matibabu zaidi ya maumivu ya goti ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu.

Kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ametumia dakika mbili pekee ilikuwa mbele ya Kagera Sugar na alianzia benchi wakati Yanga ikishinda bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum.

Pia nyota mwingine ni Kibwana Shomari beki wa kazi chafu ambaye yeye aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi hivi karibuni aliweka wazi kuwa anahitaji kuona wachezaji hao wakipelekwa Tunisia ili kupata matibabu zaidi.

“Nahitaji kuona kwamba Ninja na Kibwana wanakwenda Tunissia kama ilivyokuwa kwa Yacouba Songne ili wapate matibabu zaidi warudi kazini,”.

Tayari nyota hao wameelekea huko kupata matibabu, kila la kheri.