MASTAA YANGA WAREJEA DAR WAKITOKEA ZANZIBAR

BAADA ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi jana Januari, 10,2022 leo wamewasili Dar wakitokea Zanzibar.

Yanga iliyokuwa inatetea Kombe la Mapinduzi iliishia hatua ya nusu fainali ambapo ilipoteza kwa changamoto ya penalti dhidi ya Azam FC.

Dakika 90 zilikamilika kwa timu kutoshana nguvu bila kufungana ugumu ukawa kwenye penalti ambapo Azam ilishinda penalti 9-8 Yanga.

Miongoni mwa mastaa wa Yanga ambao walikuwa kwenye msafara ni pamoja na kipa Aboutwalib Mshery, Eric Johora,Razack Siwa ambaye ni kocha wa makipa.

Fiston Mayele, Heritier Makambo, Salim Aboubakhari na Dennis Nkane.