MFUNGAJI BORA KOMBE LA MAPINDUZI HAYUPO


JANUARI 11,2021 kiungo Miraj Athuman, ‘Sheva’ akiwa ndani ya Simba alifunga bao lake la nne katika Kombe la Mapinduzi.

Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 2-1 na Sheva aliibuka kuwa mfungaji bora.

Mwaka 2022 atakuwa kwa kideo akishuhudia tuzo yake ikisepa kwa kuwa kwa sasa anakipiga KMC kwa kuwa hayupo katika mashindano hayo mwaka huu wa 2022.

Timu ya KMC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery haijashiriki Kombe la Mapinduzi na ni Azam FC v Simba zinatarajiwa kucheza fainali, Januari 13.

Azam FC ilishinda kwenye nusu fainali ya kwanza dhidi ya Yanga kwa penalti 9-8 na Simba ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili.