VIDEO: SIRI ZITAKAZOWAMALIZA WAARABU, WALIOMSHIKA MKONO HAWA HAPA

MZEE wa saluti, shabiki wa Simba ametaja siri ambazo anaamini kwamba zitawapa matokeo chanya kwenye mchezo wa robo fainali ya pili dhidi ya Al Masri, Waarabu wa Misri mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 9 2025.

Mzee wa Saluti ni miongoni mwa mashabiki ambao walikuwa nchini Misri na walishuhudia ubao wa Uwanja wa Suez Canal ukisoma Al Masry 2-0 Simba. Shabiki huyo amewataja waliomshika mkono mpaka akakwea pipa kuelekea Misri kuishangilia Simba kwenye mchezo huo wa kimataifa uliokuwa na ushindani mkubwa.

Mbali na kupoteza Mzee wa Saluti alirejea na zawadi ambazo ilikuwa ni maalumu kwa mashabiki wa Simba ikiwa ni pamoja na shabiki maarufu kwa jina la Kinyago wa Tabata.