YANGA imewaduwaza Al Hilal kwenye mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa bao la mapema zaidi wakifunga hesabu zao kwa kusepa na pointi tatu jumlajumla wakiwa ugenini.
Bao la Aziz Ki akitumia pasi ya Dickson Job linavunja rekodi ya timu hiyo ambayo ilikuwa imecheza mechi nne bila kupoteza na inapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga.
Yanga inafikisha pointi 7 nafasi ya tatu kete yake ijayo ni dhidi ya MC Alger na Al Hilal wao watamenyana na TP Mazembe kukamilisha mechi sita katika hatua ya makundi.
Katika kusaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali, Yanga wanapaswa kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya MC Alger wakiwa Uwanja wa Mkapa.
Aziz Ki amefunga mabao mawili katika hatua ya makundi ambapo bao la kwanza alifunga kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.