SIMBA QUEENS WAIPIGA BITI YANGA PRINCES

JOTO la mechi ya Watani wa Jadi kwa upande wa soka la wanawake limezidi kutanda ambapo Yanga Princess watakuwa wenyeji wa Simba Queens katika mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye Dimba la Uhuru, Dar.


Kuelekea mchezo huo wa
raundi ya nne kunako Ligi Kuu ya Wanawake, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma ametamba kuendeleza rekodi ya ushindi dhidi ya watani zao hao.


Yanga Princess wataingia kwenye
mchezo huo wakiwa na rekodi mbaya dhidi ya Simba Queens ambapo kwenye mechi nne walizokutana, wamepoteza tatu na wameambulia sare moja.


Akizungumzia maandalizi yake
kuelekea mchezo huo, Nkoma alifunguka kwamba: “Maandalizi yanaendelea na kila mchezaji morali yake iko juu kuelekea mchezo huu.


Tunawaheshimu Yanga ni timu
nzuri na ina wachezaji wazuri, lakini malengo yetu ni kupata pointi tatu dhidi yao.

“Tuna rekodi bora dhidi yao, lakini hilo halitupi hali ya kujiamini moja kwa moja, lazima tuingie kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa bila kuwadharau wapinzani wetu.”

 

Simba Queens wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake wakiwa na pointi tisa baada ya kushuka dimbani kwenye mechi tatu wakiweka rekodi ya kuwa timu pekee msimu huu kushinda mechi tatu mfululizo

STORI: HUSSEIN MSOLEKA