AHMED Ally, Ofisa Habari wa Simba ameweka wazi kuwa malengo yake makubwa ni kuweza kuona timu hiyo inaweza kufanya vizuri zaidi kwenye ulimwengu wa mitandao ya kijamii licha ya kwamba kwa sasa inafanya vizuri zaidi pamoja na kuweza kuwazungumzia kwa ukaribu wachezaji wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na Aishi Manula, Pape Sakho na Kibu Dennis.
Simba leo inatarajiwa kucheza mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Selem View saa 10:05 jioni na tayari timu ipo huko kwa ajili ya mchezo huo ambao unasubiriwa kwa shauku na mashabiki.
Ahmed aliibuka Zanzibar muda mfupi baada ya kutanagzwa na Simba na kuweza kuanza kazi.