BORUSSIA DORTMUND YAKAMILISHA UHAMISHO WA MSHAMBULIAJI, MAXIMILIAN BEIER

Klabu ya Borussia Dortmund imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji, Maximilian Beier kwa ada ya Euro milioni 30 akitokea TSG Hoffenheim.

Beier (21) raia wa Ujerumani amesaini mkataba wa miaka mitano mpaka 2029 na anatua kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo baada ya Niclas Füllkrug kutimkia West Ham United.

Beier anatua klabuni hapo kusaidiana na ingizo jipya Serhou Guirassy huku washambuliaji Youssoufa Moukoko na Sebastien Haller wakiwa huru kuondoka klabuni.

Wakati huo huo klabu ya Olympique Marseille ipo kwenye mazungumzo na Dortmund kwa ajili ya kuipata saini ya Moukoko.