TORRES NI MALI YA BARCELONA

Nyota wa kimataifa wa Hispania Ferran Torres amekamilisha dili lake la kujiunga na FC Barcelona akitokea Manchester City dili linalotajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 61.

Torres mwenye umri wa miaka 21, anarejea Hispania baada ya miezi 18 tangia aondoke Valencia na kujiunga na Manchester City ambapo sasa ameingia mkataba wa miaka sita (2027) pamoja na kipengele cha kuondoka klabuni hapo kwa dau la pauni milioni 842 sawa na Euro bilioni moja.

Anakuwa mchezaji wa tatu baada ya Ansu Fati, na Pedro kumwaga wino wenye kipengele ghali cha kuondoka klabuni hapo chenye thamani ya bilioni moja.