Home Sports KOCHA SIMBA KUIBUKIA NAMUNGO FC

KOCHA SIMBA KUIBUKIA NAMUNGO FC

BAADA ya Hitimana Thiery aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba kuamua kuachana na mabosi hao anatajwa kuibukia Namungo FC.

Desemba 28,2021 Simba walitangaza rasmi kufikia makubaliano ya kuachana na kocha huyo.

Kwa sasa Namungo FC ipo kwenye hatua za mwisho kuweza kumtambulisha kocha wa timu hiyo baada ya Hemed Morocco kubwaga manyanga kutokana na timu hiyo kuwa katika mwendo wa kusuasua.

Jina la Hitimana ambaye aliwahi kuifundisha timu hiyo linapewa nafasi ya kuweza kuibuka tena kwa mara nyingine kuinoa timu hiyo.

Previous articleMAYANGA:TUNAPAMBANA KWA AJILI YA TIMU
Next articleTORRES NI MALI YA BARCELONA