NAMUNGO wamekomba pointi moja mbele ya Simba kwa sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo wa mzunguko wa pili, Uwanja wa Majaliwa.
Licha ya Simba kuanza kufunga kila kipindi walikwama kulinda ushindi huo mpaka dakika ya 90 huku nafasi walizotengeneza wakikwama kuzitumia ikiwa ni pamoja na ile ya Fabrice Ngoma dakika ya 90.
Willy Onana alifunga pazia la kufunga dakika ya 33 kisha Sabato Kelvin aliweka nyavuni bao dakika ya 39.
Edwin Balua alifunga kwa pigo huru dakika ya 70 na Kennedy Juma alijifunga dakika ya 90 katika mchezo huo wakigawana pointi mojamoja.