>

MWAMBA AUCHO YUPO FITI ANAPIGA MAZOEZI

KIUNGO wa kazi ndani ya Yanga Khalid Aucho mdogomdogo anazidi kurejea kwenye ubora wake akiendelea na mazoezi kwa ajili ya kuwa tayari kwa mechi za ushindani kitaifa na kimataifa. Nyota huyo alikosekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns kwa kuwa alikuwa hajafikia asilimia 100 ya kuwa tayari kwa mapambano kwenye mchezo huo waliotoshana nguvu bila kufungana.