Klabu ya Yanga imeripotiwa kuwa ukingoni kukamilisha dili la kumsajili kiungo mkata umeme kutoka Ivory Coast, Djire Abdoulaye kutoka klabu ya Racing Club Abidjan. Young Africans SC inahitaji kiungo mwingine mkabaji haraka iwezekanavyo ikiwa ni pendekezo la kocha Miguel Gamondim
Abdoulaye (17) anatazamiwa kukubaliana pia masharti ya kibinafsi na Young Africans licha ya msururu wa vilabu kadhaa vikiwemo ASEC Mimosas na TP Mazembe vinavyowania saini yake.
Yanga SC inatarajia kuwasilisha ofa hivi karibuni ambapo zaidi dola 120,000 zinatarajiwa kuwatoka kwa ajili ya kuinasa saini ya kinda huyo anayefananishwa na Mohammed Zougrana ambaye alitimkia MC Algiers baada ya Wananchi kuzidiwa kete.