TANZANITE QUEENS TAYARI KUWAKABILI NIGERIA

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Wasichana chini ya miaka 20, Tanzanite Queens wanaendelea na maandalizi ya mwisho.

Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu Bakari Shime ina kibarua cha kusaka ushindi mchezo dhidi ya Nigeria.

Huo ni mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Novemba 12.

Ikumbukwe kwamba Tanzanite Queens waliwafungashia virago Djibouti Kwa jumla ya mabao 12-0.

Shime ameweka wazi kuwa maandalizi yanaendelea vizuri kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.