YANGA KAZI BADO INAENDELEA

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kazi bado inaendelea kwenye mechi za kitaifa na kimataifa lengo ikiwa ni kupata matokeo chanya.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi sita na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 10.

Licha ya kuwapa mazoezi kwenye kambi ya AVIC pia Gamondi aliwapeleka vijana wake ufukweni kuendelea na mazoezi.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliopo kwenye mazoezi ni pamoja na Farid Mussa, Maxi Nzengeli.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika ni hatua ya pili inakwenda kucheza baada ya kuwafungashia virago ASAS FC ya Djiout kwa jumla ya mabao 7-1.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa kazi inaendelea kwenye kila hatua ambayo wapo.

“Kila siku tunahitaji kuwa bora, msimu uliopita tulionyesha ushindani kwenye ligi na kutwaa ubingwa na kwenye mashindano ya kimataifa rekodi iliandikwa kwa kufika fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

“Msimu mwingine tena tunaendelea pale ambapo tuliishia kazi haijaisha bado tupo imara. Mashabiki wamekuwa pamoja nasi waendelee katika hilo kwani uwepo wao ni muhimu,” amesema Kamwe.