AZAM FC WASHINDI WA TATU NGAO YA JAMII

AZAM FC chini ya Kocha Mkuu, Yusuph Dabo ni washindi wa tatu Ngao ya Jamii baada ya kuwashinda Singida Fountain Gate.

Ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga umesoma Azam FC 2-0 Singida Fountain Gate.

Mabao ya Prince Dube na Sopu yametosha kuimaliza Singida Fountain Gate.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Dabo kushuhudia timu hiyo ikipata ushindi Tanga baada ya ule wa kwanza hatua ya nusu fainali kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga.

Yanga imetinga fainali na inatarajia kucheza na Simba kwenye mchezo wa fainali Uwanja wa Mkwakwani, Tanga saa 1:00 usiku.