Home Sports YANGA V SIMBA, HII GEMU HAINA MWENYEWE

YANGA V SIMBA, HII GEMU HAINA MWENYEWE

WEKA ngoma ipigwe wanasema tumewafuata waliotangulia ni kueleka mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga  V Simba.

Kila timu ina nyota wapya ikiwa ni pamoja na Jonas Mkude, Skudu Makudubela na Maxi Nzengeli kwa Yanga, Luis Miquissoe, Willy Onana kwa Simba.

Ikumbukwe kwamba Yanga waliitungua mabao 2-0 Azam FC kisha Simba wao walipenya kwa ushindi wa penalty 4-2 Singida Fountain Gate hivyo kila mmoja anatambua anachokisaka uwanjani.

Hapa  tunakuletea namna kazi itakavyokuwa namna hii:-

Wakali wa kazi wamerudi

 Jesus Moloko wa Yanga adhabu ya kadi nyekundu aliyopata mchezo dhidi ya Mbeya City imeisha baada ya kuzikosa mechi tatu hivyo ataiwahi Simba fainali Ngao ya Jamii.

Moloko alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Azam FC hizi zilikuwa kwenye ligi msimu wa 2022/23 na Yanga v Azam FC huu ulikuwa mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkwakwani.

Nyota huyo alitoa jumla ya pasi tano za mabao kwenye ligi huku akifunga mabao mawili alipokomba dakika 1,403 katika mechi 23 ambazo alipata nafasi ya kucheza.

Clatous Chama wa Simba adhabu ya kufungiwa mechi 3 baada ya kumchezea faulo Abal Kassim wa Ruvu Shooting imeisha hivyo ataiwahi Yanga fainali ya Ngao ya Jamii

Chama alikosa mechi tatu ambazo ni  Simba v Polisi Tanzania, Simba v Coastal Union hizi zilikuwa za ligi msimu wa 2022/23 na Simba v Singida Fountain Gate hii ilikuwa kwenye Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali ya pili, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ni adhabu kutoka Kamati ya Usimamizi wa Ligi Kuu Bara alikutana nayo kinara huyo wa pasi za mwisho alipotoa 14 na kutupia mabao manne kwenye ligi. Ni mechi 21 alicheza akikomba dakika 1,913.

Dakika 180 Simba majanga

Katika mechi mbili za Ngao ya Jamii Simba iliangukia pua mbele ya Yanga Uwanja wa Mkapa. Kete ya kwanza ilikuwa Septemba 25 2021 ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga na kipa alikuwa ni Aishi Manula mtupiaji alikuwa Fiston Mayele dakika ya 69.

Ngoma ya pili ilikuwa Uwanja wa Mkapa Agosti 13 ubo ulisoma Yanga 2-1 Simba. Ni Pape Sakho wa Simba alifunga dakika ya 14 kisha Fiston Mayele alitupia mabao mawili kwa Yanga dakika ya 49 na 80.

Ndani ya dakika 180 Simba hawakuwa na bahati na Yanga kwa kutunguliwa jumla mabao matatu na kupishana na mataji mawili ya Ngao ya Jamii.

Mbali na kupishana na mataji ya Ngao ya Jamii pia hata taji la ligi nalo walikuwa ni mashuhuda likielekea kwa watani zao wa jadi Yanga. Mayele na Pape ipo wazi kuwa hawatakuwa kwenye kikosi cha leo baada ya kupata changamoto mpya.

Kadi njenje

Kwenye beto ya Kariakoo Dabi kadi huwa hazikosekani, rekodi zinaonyesha kuwa Septemba 25 2021 Ramadhan Kayoko ambaye alikuwa ni mwamuzi wa kati alitoa jumla ya kadi 8 za njano huku akitoa kadi moja nyekundu kwa Thadeo Lwanga ilikuwa ni baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Agosti 13 ni Elly Sassi alikuwa refa wa kati alimuonyesha kadi ya njano Feisal Salum ilikuwa dakika ya 87, Salim Aboubhakari, (Sure Boy) dakika ya 45, Bernard Morrison ilikuwa dakika ya 90 hawa ni kwa upande wa Yanga na Henock Inonga dakika ya 45, Sadio Kanoute dakika ya 59.

Hili gemu halina mwenyewe

Gemu la leo halina mwenyewe kwa kuwa mfalme Mayele aliyekuwa na zali la kuwatungua Simba hayupo na Sakho aliyepata zali la kuwafunga Yanga hayupo.

Pia zali huwa linawatokea wachezaji wakati mwingine kama ilivyokuwa Zawadi Mauya aliyewatungua Simba, Kibu Dennis wanamuita mkandaji aliyewatungua Yanga hivyo mwenye bahati litakuwa gemu lake na dakika 90 zitaamua.

Previous articleAZAM FC WASHINDI WA TATU NGAO YA JAMII
Next articleWAKALI WA PASI NDEFU YANGA NA SIMBA KWENYE VITA NYINGINE