DAU LA HAALAND LAFICHWA

DAU la nyota kikosi cha Borussia Dortmund, Erling Haaland ambaye anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Real Madrid limefichwa kwa wakati huu.

Ripoti zinaeleza kuwa Haaland mpaka sasa bado hajafanya maamuzi ya wapi atakuwa kwa ajili ya kupata changamoto mpya licha ya timu nyingi kutajwa kuwania saini yake ili kuweza kumpata mshambuliaji huyo

Mabosi wa Borussia Dortmund wamegoma kuweka wazi mkwanja ambao wanahitaji kuupata kwa wakati huu ili waweze kumuuza mchezaji huyo.

Awali mkwanja ambao uliokuwa unatajwa kumpata nyota huo ni kati ya Euro milion 70 mpaka 100 huko ila haijawekwa wazi.