SINGIDA FOUNTAIN GATE FC NI ARUSHA

RASMI Klabu ya Singida Fountain Gate ya Singida imebainisha kuwa kambi yake itakuwa ni Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Singida Fountain Gate FC imeeleza namna hii:”Tunapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wa Singida Fountain Gate FC kwamba maandalizi ya msimu ujao kwa klabu yetu yatafanyikia jijini Arusha kuanzia Julai 10, 2023.

“Awali maandalizi yalikuwa yafanyikie kwenye nchi ya Tunisia lakini kutokana na ufinyu wa muda na kuchelewa kukamilika kwa zoezi la usajili wa wachezaji, tumelazimika kubaki nchini ili wachezaji wote waweze kushiriki maandalizi haya kwa wakati,”.

Tayari timu hiyo imeanza kuwapa mkono wa asante wachezaji wao pamoja na kuwaongezea mikataba wachezaji ikiwa ni pamoja na Bruno Gomes, Benedict Haule hawa bado wapo ndani ya kikosi hicho.