WATATU WATAMBULISHWA NDANI YA SIMBA

KATIKA maboresho ya benchi la ufundi kikosi cha Simba kimeongeza watu watatu Kwa ajili ya msimu wa 2023/24.

Ni Corneille Hategekimana huyu ni kocha mpya wa viungo ndani ya Simba yeye ni raia wa Rwanda na amewahi kufanya kazi ndani ya Vipers.

Pia Daniel Cadena ambaye alikuwa ndani ya Azam FC huyu atakuwa ndani ya Simba kitengo cha makipa.

Na mwamba mwingine ni Mikael Igendia huyu ni Meneja mpya na mkuu wa Sayansi ya Michezo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Simba amesema kuwa wanahitaji kufanya maboresho makubwa kwenye benchi la ufundi pamoja na timu kiujumla.

“Tulikuwa tuna idadi ya ambao wamepungua kwenye benchi la ufundi hivyo tunakwenda kufanya maboresho makubwa na malengo ni kuona tunakuwa imara kila idara,” .