MBEYA City wamekubali kugawana pointi mojamoja na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Sokoine.
Ni Mbeya City walitangulia kufunga mabao mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa George Sangija dakika ya pili na lile la pili likifungwa na Richardson Ng’odya aliyefunga mabao mawili.
Bao la pili alifunga dakika 53 ikiwa ni kipindi cha pili na Yanga waliweka usawa kupitia kwa Bernard Morrison dakika ya 64 kwa mkwaju wa penalti.
Sure Boy alipachika bao la pili dakika ya 68 wakati Mbeya City wakisubiri mpira uishe Morrison aliwatungua bao dakika ya 90.
Wachezaji wawili wameonyeshwa kadi nyekundu Hassan Nassoro wa Mbeya City na Jesus Moloko wa Yanga dakika ya 87.