UBAO wa Uwanja wa Azam Complex unasoma Simba 3-0 Polisi Tanzania.
Ni mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kukamilisha msimu wa 2022/23.
Ni mabao ya Saido Ntibanzokiza ambaye amefunga hatrick ndani ya dakika 10 za mchezo huo.
Nyota Jean Baleke amekwama kusepa na dakika 90 baada ya kupata maumivu dakika ya 15 nafasi yake ikichukuliwa na nahodha John Bocco.
Ntiba amefunga mabao hayo dakika ya 15, 20 na dakika ya 26.