Home Sports NABI AFURAHIA MASHABIKI WA MARUMO

NABI AFURAHIA MASHABIKI WA MARUMO

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema wanapenda kucheza na mashabiki hivyo jambo ambalo wapinzani wao wamefanya ni zuri.

Leo Yanga inatarajiwa kutupa kete kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambao watakuwa nyumbani.

Kwenye mchezo wa leo wapinzani wao wamefuta kiingilio wakihitaji kuwa na mashabiki wengi ili wafanikishe malengo ya kupindua meza katika mchezo wa leo.

Ipo wazi kwamba katika mchezo wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-0 Marumo hivyo Yanga imetanguliza mguu mmoja kutinga hatua ya fainali ikiwa italinda ushindi ama kuongeza idadi ya mabao.

Nabi amesema:”Ni jambo zuri Marumo wamepanga mechi isiwe na kiingilio. Sisi kama Yanga tunapenda kucheza mbele ya mashabiki wengi kuliko uwanja kukosa mashabiki. Nina wachezaji wenye uzoefu wa kutosha wa kucheza mechi za namna hii”

Previous articleWAKALI WA PASI ZA MWISHO BONGO HAWA HAPA
Next articleKAPOMBE BADO HAJAPATA MBADALA WAKE SIMBA