KAPOMBE BADO HAJAPATA MBADALA WAKE SIMBA

SHOMARI Kapombe beki wa kazi ndani ya kikosi cha Simba ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Roberto Oliveira.

Pasi yake ya sita kwenye ligi ilikuwa dhidi ya watani wa jadi, Yanga Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-0 Yanga.

Ikiwa hatakuwa fiti hapo ni pasua kichwa kwa kuwa mbadala wake ni Israel Mwenda ambaye naye msimu huu amekuwa nje akipambania hali yake.

Kwenye eneo hili ni muhimu Simba kumtafuta mtu wa kazikazi ili kupata nafasi ya kuwa na nyota zaidi ya wawili kwenye kikosi hicho,

Ndani ya Ligi Kuu Bara Kapombe yupo imara kwenye kupandisha mashambulizi na anajua kufunga pia.

Ni pasi sita kibindoni anazo ndani ya timu hiyo ambayo imegotea nafasi ya pili kwenye ligi na katika Ligi ya Mabingwa Afrika ni hatua ya robo finali.

Timu ya Simba imekosa kila taji ililokuwa inapambania kwa msimu wa 2022/23.