BAADA ya Geita Gold kuambulia kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga ,Mkurugenzi wa Geita Gold Zahar Michuzi amefunguka na kusema kuwa Yanga waliwapangia kikosi cha CAF.
Mchezo huo ulipigwa wikiendi hii Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi ambapo Geita Gold ilianza kufunga kisha ikakwama kushinda mchezo huo.
Mwenyeketi wa Geita Gold Zahar amesema “Kitendo cha Yanga kutuwekea kikosi cha CAF kwa timu yetu ya Geita Gold iliyotoka Buseresere ni shambulio la aibu kwa sababu haiwezekani kikosi cha CAF tuchezeshwe sisi utafikiri wanacheza Shirikisho?
“Kulikuwa na haja gani ya kufanya hayo yote hayo tunaweza tunawamudu isipokuwa bahati ili kuwa siyo kwetu mchezo ulikuwa mzuri pande zote lakini sisi tulikosa matokeo,” .
Geita Gold imepoteza mechi zote mbili dhidi ya Yanga ule wa awali ilifungwa bao 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba na mzunguko wa pili walifungwa mabao 3-1.