GEITA GOLD, SINGIDA BIG STARS ZAPETA

MAPEMA leo kwenye mechi za hatua ya 16 bora Kombe la Azam Sports Federation Geita Gold walikata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Ni ushindi wa mabao 3-1 wameupata dhidi ya Green Warriors kwenye mchezo huo.

Geita Gold imeweka wazi kuwa hesabu zake ni kutinga hatua ya fainali ya kombe hilo ambalo bingwa mtetezi ni Yanga.

Pia Singida Big Stars nao wamepenya katika hatua ya 16 bora kwa ushindi wa bao 1-0 walilopata dakika za usiku dhidi ya JKT Tanzania.