WATATU KUIKOSA IHEFU KESHO

KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Ihefu mastaa watatu wanatarajiwa kuukosa mchezo huo.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi kesho Januari 16 ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Ihefu.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Highland State ulisoma Ihefu 2-1 Yanga.

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedrick Kaze amesema kuwa miongoni mwa watakaokosa mchezo huo ni Bernard Morrison, Aziz KI na beki Yannick Bangala.