KWENYE mchujo wa fainali yao katika msako wa kocha bora mwezi Desemba 2022 ni mzawa Juma Mgunda kasepa na tuzo hiyo.
Kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa kikao cha majadiliano kilifanyika Januari 7,Desemba 2023.
Mgunda amewashinda wageni Hans Pluijm na Nasreddine Nabi ambao aliingia nao fainali katika hilo anastahili pongezi.
Pia kwa upande wa mchezaji bora wa Desemba 2022 ni Clatous Chama ambaye anafundishwa na Mgunda kamshinda nahodha wake John Bocco.
Kutoka Yanga ni mzee wa kutetema Fiston Mayele yeye aliingia kwenye fainali hiyo.
Kwa maana hiyo kwenye orodha ya watu sita waliofanya vizuri kwa mwezi Desemba wazawa wamepenya wawili pekee na wageni wakiwa wanne, kazi iendelee 2023.