KIUNGO mzawa ndani ya kikosi cha Simba, Mzamiru Yassin ni mvivu,mvivu,mvivu haswa kwenye kuongea lakini akiwa uwanjani anavunja jasho kwelikweli.
Mara chache kumkuta akizungumza na hata akizungumza hana maneno mengi zaidi ya tunasmhurku Mungu na maandalizi yapo vizuri.
Eneo lake la kati kwenye ukabaji bado Simba haina mbadala wake mzawa ikiwa atasepa kwenye kikosi cha Simba kupata changamoto mpya.
Hana nyimbo nyingi uwanjani zaidi ya kuongea kwa miguu huku mikato ya kimyakimya kwake likiwa ni jambo ambalo halikwepeki kama ilivyo kwa mshikaji wake Sadio Kanoute.
Mchezo wake wa funga mwaka 2022 alikuwa kwenye ubora wake dhidi ya Tanzania Prisons na alitoa pasi mbili za mabao.
Kazi bado inaendelea msimu wa 2022/23 haujameguka ni muda wa wazawa kuongea kwa vitendo zaidi.