MRITHI WA OLE ATAJWA KUWA ZIDANE

BAADA ya Manchester United kumfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer jina la Zinadine Zidane linatajwa kuwa miongoni mwa makocha watakaorithi mikoba ya kuinoa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Solskjaer mchezo wake wa mwisho kukaa kwenye benchi akiwa ni kocha mkuu ilikuwa ni dhidi ya Watford na alishuhudia timu hiyo ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 na anatajwa kwamba aliwaaga wachezaji wake tayari.

Ripoti zimeeleza kuwa bosi wa United,Joel Glazer huyu amepewa kazi ya kuhakikisha kwamba anampata Zidane ambaye kwa sasa hana timu baada ya kumalizana na mabosi wa Real Madrid ikiwa ni timu pekee aliyopata nafasi ya kuifundisha kwenye maisha yake ya kazi ya ukocha.

Ikiwa dili la Zidane litabuma basi hesabu zinatajwa kuhamia kwa Brendan Rodgers ambaye anainoa Leicester City ambapo kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Michael Carrick ambaye ataongoza timu hiyo kwa muda kabla ya kupatikana kwa kocha ambaye ataendeleza majukumu ya kuinoa timu hiyo.