>

MOROCCO WAMEMALIZA MWENDO WA KUSAKA FAINALI

MWENDO wa Timu ya Taifa ya Morocco kutoka Afrika umegotea hatua ya nusu fainali baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa.

Ufaransa imewafunga Morocco mabao 2-0 sasa itamenyana na Timu ya Taifa ya Argentina kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022 inayotarajiwa kuchezwa Jumapili.

Ni mabao ya Theo Hernandez dakika ya 5 likiwa ni bao la mapema lililowavuruga Morocco na bao la Randal Kolo Muani dakika ya 79.

Hili linakuwa ni bao la kwanza kwa Randal la mashindano kufunga akiwa na timu ya taifa.

Jitihada za mastaa wa Morocco kusaka ushindi ikiwa ni pamoja na Jawad El Yamiq ziligonga mwamba kwenye mchezo huo na kuwafanya kushindwa kufikia malengo ya kucheza fainali.