KIUNGO wa Yanga, Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji ambao wataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Namungo FC.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ilulu, Lindi.
Sababu kubwa ya nyotahuyo kukosa mchezo huo ni majeraha ambayo aliyapata kwenye mguu wa kulia alipokuwa akiitumikia timu ya taifa ya Uganda.
Wengine ambao wataukosa mchezo wa kesho ni pamoja na Ramadhan Kabwili, Dickson Ambundo na Balama Mapinduzi.