ANFIELD LIVERPOOL YABAKI NA POINTI ZOTE TATU

WAKIWA Uwanja wa Anfield, Liverpool walipindua meza kwa kuwa walifungwa bao la mapema na Alexander Isak dakika ya 38 nyota wa Newcastel United.

kipindi cha pili mabao ya Roberto Firmino dakika ya 61 na bao la ushindi lilifungwa na Fabio Carvalho dakika ya 90+8 na kuwafanya wabaki na pointi zote tatu muhimu.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha pointi 8 ikiwa nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Newcastel United wao wanabaki na pointi 6 wakiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo baada ya mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Mashuti ambayo Liverpool ilipiga kuelekea lango la wapinzani wao yalikuwa ni 23 huku Newcastel United wao wakipiga mashuti matano.

Ni sita ambayo yalilenga lango kwa Liverpool na mawili yalilenga lango kwa Newcastel United.