Home Uncategorized YANGA YAIVUTIA KASI AZAM FC

YANGA YAIVUTIA KASI AZAM FC

KIKOSI cha Yanga kipo kwenye maandalizi ya mchezo wao wa ligi ujao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6,2022 Uwanja wa Mkapa.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye ameongoza kwenye mechi mbili za ligi bila kuonja ladha ya kupoteza.

Ilikuwa mchezo wake dhidi ya Polisi Tanzania iliposhinda mabao 2-1 na mchezo wao dhidi ya Coastal Union waliposhinda mabao 2-0 mechi zote zilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Nabi ameweka wazi kuwa mchezo huo utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya kusaka matokeo ndni ya daika 90.

“Tunatambua kwamba kila mechi ni ngumu na ushindani kwenye ligi ni mkubwa hivyo tutajitahidi kupata ushindi kwa ajili ya kuzidi kuwa imara zaidi kupambania taji la ligi na kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.

Kwa upande wa Azam FC, Ofisa Habari wa timu hiyo Zakaria Thabit amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo watajitahidi kupambana kupata ushindi.

“Maandalizi yanaendelea na tupo tayari kwa ajili ya mechi zote wachezaji wapo tayari,” amesema.

Azam FC imepata ushindi kwenye mechi moja na kulazimisha sare kwenye mchezo mmoja wa ligi msimu wa 2022/23.

Previous articleANFIELD LIVERPOOL YABAKI NA POINTI ZOTE TATU
Next articleMKE WA GAEL BIGIRIMANA HUYU HAPA MZUNGU